Ripoti mpya ya KNBS iliyotolewa Jumatatu inaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, visa vya uhalifu na wizi wa kimabavu vimeongezeka mara dufu kutokana na gumu wa kimaisha unaozidi kuwakung’uta maelfu ya Wakenya hasa vijana wasio na ajira.
Utafiti unaonyesha kuwa kuna uhalifu zaidi unaoripotiwa kote nchini; inaonyesha kuwa kesi 104,842 za uhalifu ziliripotiwa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.
Hii ni kutokana na ugumu wa kimaisha kutokana na hali ya uchumi kuzidi kuwa mbaya na vijana wengi kutokuwa na ajira wa kuwakimu kimaisha, wengi kuishia katika shughuli za kufanya wizi - njia hatarishi ya kujitafutia riziki.
Ongezeko la uhalifu nchini linalingana na kesi zilizoko mahakamani, na rekodi ya kesi 649,229 katika mahakama ambazo bado hazijahitimishwa, na ongezeko la idadi ya wafungwa nchini kutoka wafungwa elfu 169 mnamo 2022 hadi 248,000 mwaka jana.
Sekta ya elimu nchini pia imerekodi ukuaji huku idadi ya wanaoandikishwa ikiongezeka katika viwango vyote vya elimu nchini Kenya.
Katika kipindi hicho, uandikishaji katika shule za msingi, chekechea, sekondari, TVET na vyuo vikuu vyote vilirekodi ongezeko.
Ongezeko la idadi ya wanafunzi wa TVET na vyuo vikuu pia linakwenda sambamba na ongezeko la kiasi cha fedha zinazotolewa kwao kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Mwaka jana, serikali ilitoa faida ya mkopo kutoka Ksh.10.6 bilioni hadi Ksh.31.8 bilioni.
Inatarajiwa pia kuwa idadi ya wanafunzi wanaotafuta huduma hizi za kifedha inatarajiwa kuongezeka mwaka huu.