Waandamanaji waharibu na kupora klabu ya Timba XO inayohusishwa na Oscar Sudi

Klabu hiyo inayojulikana kama Timber XO iko kando ya barabara ya Eldoret- Nairobi.

Muhtasari

•Klabu hiyo ilifunguliwa rasmi wiki chache wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Sudi na wabunge wengine kadhaa.

Waandamanaji mjini Eldoret walivamia, kuharibu na kupora klabu moja mjini Eldoret inayohusishwa na mbunge wa kapseret Oscar Sudi.

Klabu hiyo inayojulikana kama Timber XO iko kando ya barabara ya Eldoret kuelekea Nairobi. Klabu hiyo ilifunguliwa rasmi wiki chache zilizopita wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Sudi na wabunge wengine kadhaa

Waandamanaji hao waliandamana kutoka Eldoret CBD hadi kwenye klabu ambapo walivamia na kuharibu kuta za vioo, madirisha na milango.

Polisi walifika huku baadhi ya waandamanaji wakiingia kwenye klabu na kuondoka na baadhi ya vitu.