Tazama maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumatano- KPLC

KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo

Muhtasari

•KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 3. 

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Nyeri, Tharaka Nithi.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 3. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Nyeri, Tharaka Nithi.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu kadhaa za mtaa wa Eastleigh zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Chiga katika kaunti ya Kisumu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.

Sehemu kadhaa za soko ya Gikumbo na soko ya Gaikuyu zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Tharaka Nithi, sehemu kadhaa za maeneo ya Chuka na Kimbumbu yatokosa umeme kati ya saa mbili unusu na saa kumi na moja jioni.