logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Alhamisi - KPLC

Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

image
na SAMUEL MAINA

Habari11 July 2024 - 05:11

Muhtasari


  • •Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
  • •Katika kaunti ya Nairobi, mtaa wa Gigiri Whispers utaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Julai 11. 

Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Nairobi, Kajiado, Nyeri, Embu, Kiambu, na Kilifi.

Katika kaunti ya Nairobi, mtaa wa Gigiri Whispers utaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Loitokitok katika kaunti ya Kajiado zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Ndunyo na Mahiga katika kaunti ya Nyeri zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za eneo la Majengo katika kaunti ya Embu pia zithakosa umeme kati ua saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Katika kaunti ya Kiambu, mtaa wa Riara na hospitali ya Nazareth zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za eneo la Ganze katika kaunti ya Kilifi pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved