Wakenya wazungumzia baridi iliyotanda jijini Nairobi

"Watu wa Nairobi hii ni baridi ama ni fridge...?" Stephen Letto alihoji.

Muhtasari

•Mtayarishaji wa maudhui Azziad Nasenya kupitia ukurasa wa Instagram aliandika;"Hii baridi ya leo iko na PHD juu wueeh"

•Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya ilionya wakenya kujiandaa kutokana  na mvua kubwa zaidi mnamo Julai ambayo inaweza kugeuka kuwa mvua ya mawe mnamo Agosti.

Image: BBC

Baadhi ya wakenya wameibua wasiwasi kuhusu baridi ambayo imeenea kote jijini Nairobi hii leo Alhamisi Julai 18,2024.

Mwanatiktok na mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali, Azziad Nasenya kupitia ukurasa wa Instagram aliandika;

"Hii baridi ya leo iko na PHD juu wueeh"

Kwa upande mwingine mwanahabari wa runinga ya Citizen Stephen Letoo ,kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika;

"Watu wa Nairobi hii ni baridi ama ni fridge...?"

siku ya Jumapili, Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya ilionya wakenya kujiandaa kutokana  na mvua kubwa zaidi mwezi Julai ambayo inaweza kugeuka kuwa mvua ya mawe mnamo Agosti.

Idara hiyo ilieleza kuwa mvua ya Julai sio ya kawaida na kwamba ilisababishwa na mwingiliano wa hewa baridi kutoka mashariki na hewa ya joto kutoka magharibi.

"Si ajabu kupata mvua mwezi Julai nchini Kenya. Hii hutokea wakati hewa baridi kutoka mikoa ya kati na mashariki, ikiwa ni pamoja na Nairobi, inapoingiliana na hewa yenye unyevunyevu kutoka magharibi."

"Hewa yenye uvuguvugu hupanda juu ya hewa baridi, na kusababisha mvua kubwa," idara hio ilieleza.