logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumatatu

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Bomet, Trans Nzoia, Kisii,Nyamira, na Nyeri.

image
na SAMUEL MAINA

Habari22 July 2024 - 04:41

Muhtasari


  • •Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanywa kwenye mitambo.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Bomet, Trans Nzoia, Kisii,Nyamira, na Nyeri.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Julai 22. 

Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanywa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Bomet, Trans Nzoia, Kisii,Nyamira, na Nyeri.

Katika kaunti ya Bomet, sehemu kadhaa za maeneo ya Kiromwok na Kitoben yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Kaplamai na Nyakinywa katika kaunti ya Trans Nzoia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Kisii, sehemu za eneo la Mogumo zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu za mji wa Nyamira na Kebirigo katika kaunti ya Nyamira zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhina saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Chorongi na Skuta katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved