logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DCI wamkamata msaidizi wa chifu kwa kumnajisi mtoto wa miaka 4

Chifu Msaidizi, 42, anadaiwa kumnajisi msichana huyo wa miaka minne.

image

Habari23 July 2024 - 14:12

Muhtasari


  • Kulingana na taarifa ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), mwanamume huyo alikamatwa baada ya wazazi wa mtoto huyo kuripoti kisa hicho.
Mwanaume aliyekamatwa

Maafisa wa upelelezi huko Kuresoi wamemtia mbaroni msaidizi wa chifu kwa madai ya unajisi.

Chifu Msaidizi, 42, anadaiwa kumnajisi msichana huyo wa miaka minne.

Kulingana na taarifa ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), mwanamume huyo alikamatwa baada ya wazazi wa mtoto huyo kuripoti kisa hicho.

"Kukamatwa huko kulifuatia ripoti ya kuhuzunisha kutoka kwa wazazi wa mtoto mwenye umri wa miaka 4 ambaye alikuwa amelalamikia maumivu makali wakati wa kukojoa na kuwafanya wazazi wake kuchunguza zaidi," DCI alisema.

DCI alisema mtoto huyo alifichua kuwa alinajisiwa na mshukiwa na kusababisha wazazi hao kumpeleka hospitalini mara moja ili kuchunguzwa na kutibiwa.

DCI ilisema baada ya kupokea ripoti hiyo, uchunguzi wa kisa hicho ulianza na kupelekea mshukiwa kukamatwa.

Mshukiwa huyo amefikishwa mahakamani na kwa sasa amezuiliwa Nakuru.

DCI ilisema kuwa kesi hiyo itatajwa Julai 25, 2024.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved