logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza kaunti 4 zitakazoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Jumatatu

Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nandi, Nyamira, Nyeri na Kirinyaga.

image
na SAMUEL MAINA

Habari29 July 2024 - 04:28

Muhtasari


  • •KPLC Ilisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nandi, Nyamira, Nyeri na Kirinyaga.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Julai 29. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nandi, Nyamira, Nyeri na Kirinyaga.

Katika kaunti ya Nandi, maeneo ya Chebilat na Aldai Technical yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa nne asubuhi na saa sita adhuhuri.

Eneo la Tombe Tea Factory katika kaunti ya Nyamira litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Skuta na Thunguma katika kaunti ya Nyeri zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Sehemu kadhaa za maeneo ya Thumaita na Mucagara katika kaunti ya Kirinyaga pia zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved