logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rais Ruto aahidi kuongeza wafanyikazi ili kuharakisha ujenzi wa uga wa Talanta

Alisema serikali inaboresha miundombinu mbalimbali ya michezo ili kutoa mafunzo bora kwa wanamichezo

image
na Davis Ojiambo

Habari31 July 2024 - 07:16

Muhtasari


  • •Rais Ruto alikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo-Talanta ,jijini Nairobi Julai 30,2024.
  • •Rais alidai kuwa mradi huo utafafanua upya wasifu wa michezo wa Kenya na kusababisha kituo cha kipekee na uboreshaji wa miundombinu kwa jiji la Nairobi na taifa.
Rais William Ruto

Rais William Ruto alikagua  maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo wa Talanta,jijini Nairobi.

Kwenye ziara yake ,Jumanne alasiri rais alisema kuwa  uwanja  huo wa michezo utakamilika kabla ya mwisho wa mwaka ujao tayari kuandaa kombe la mataifa ya Afrika (Afcon) mnamo 2027.

“Nimekuja hapa leo kukagua maendeleo ya kazi za ujenzi wa uwanja huu. Tutaajiri watu wengi zaidi ili kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kabla ya mwisho wa mwaka ujao,” Rais alisema.

Uwanja huo  unatazamiwa kutumika kwenye mechi mbali mbali za Afcon 2027.

Rais pia alisema kuwa mradi huo utafafanua upya wasifu wa michezo wa Kenya na kusababisha kituo cha kipekee na uboreshaji wa miundombinu kwa jiji la Nairobi na taifa.

Alibainisha kuwa Kenya ina nia ya kuendeleza na kutekeleza mpango kabambe wa miundombinu ya sekta ya michezo na ubunifu.

Alisema serikali inaboresha miundombinu mbalimbali ya michezo ili kutoa mafunzo bora kwa wanamichezo na wakati huo huo, kukuza vipaji vya michezo nchini kote.

Muundo uliozinduliwa na serikali miezi michache iliyopita unaonyesha kituo hicho kitakuwa na vyumba vya kubadilishia nguo kwa ajili ya timu na wasimamizi wa mechi.

Pia kutakuwa na utoaji wa vyumba vya matibabu, chumba cha kudhibiti vipimo vya wachezaji na maeneo yanayohusiana na watazamaji, sehemu ya watu mashuhuri, sehemu ya  vyombo vya habari, na maeneo mengi  ya utangazaji. Zaidi ya hayo, serikali itajenga miundombinu ya ICT na maeneo ya maegesho.

Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) linataka uso wa uwanja uwe wa kijani kibichi, usawa, na uwekwe alama nyeupe. Alama kwenye uwanja zinapaswa kuwa linganifu katika uwanja wote wa mchezo.

Kabla ya hapo, Rais Ruto alikuwa  ametembelea shule ya msingi ya Lenana, ambako madarasa zaidi yanajengwa ili kukidhi ongezeko la wanafunzi katika taasisi hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved