KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Julai 31.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kiambu, Homabay, Kisii, Migori, Meru, na Mombasa.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Mwiki, Githurai 44, na Zimmerman zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Raiyani, Kahuguini, na Nembu katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Baadhi ya sehemu za maeneo ya Riosiri na Nyamarambe katika kaunti ya Kisii zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Ringa na Kadongo katika kaunti ya Homabay pia yataathirika wakati huohuo.
Katika kaunti ya Migori, maeneo ya Ntimaru na Masangora yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Sehemu za maeneo ya Kinoru na Kirogine katika kaunti ya Meru pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu ya mji wa Nyali katika kaunti ya Mombasa zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.