KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme Ijumaa

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Agosti 2.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC imesema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Makueni, Homa Bay, Kisii, na Migori.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Agosti 2. 

Katika taarifa ya Alhamisi jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Makueni, Homa Bay, Kisii, na Migori.

Katika kaunti ya Makueni, sehemu za Mombasa Road zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Ibacho na Riamakanda katika kaunti ya Kisii yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Homabay, sehemu za maeneo ya Misambi, Othoro, Ooodi Beach na Agolo Muok zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Eneo la Lwanda Magwar katika kaunti ya Migori litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.