logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PS wa masuala ya Kigeni, Korir Sing’oei aitaka serikali kudhibiti maandamano kwa uthabiti

Matamshi yake yanakuja siku moja tu kabla ya vijana wa Kenya kupanga kuandamana kwa lengo la kusukuma mageuzi na mapinduzi nchini Kenya

image
na Samuel Maina

Habari06 August 2024 - 13:39

Muhtasari


  • •“Sehemu ya sababu ya kudhibiti na kushughulikia maandamano yenye ghasia na machafuko ni kwamba waandamanaji hawatambui gharama za vitendo vyao,” alisema.

Katibu Mkuu wa Masuala ya Kigeni, Korir Sing’oei, sasa anataka Serikali kudhibiti kwa uthabiti mikutano na maandamano nchini Kenya akitaja changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na shughuli hizi.

Katika taarifa kwenye akaunti yake ya X, PS huyo alibainisha kuwa maandamano, mara nyingi yanayojumuisha kaumu kubwa ya watu, yameathiri uchumi hasa katika sekta binafsi.

“Sehemu ya sababu ya kudhibiti na kushughulikia maandamano yenye ghasia na machafuko ni kwamba waandamanaji hawatambui gharama za vitendo vyao,” alisema.

“Gharama hii inahamishiwa na kubebeshwa mtu mwingine - sekta binafsi. Kama uchafuzi wa mazingira, maandamano yenye ghasia yanapaswa kudhibitiwa kabla hayajasababisha gharama za umma zisizoweza kurekebishwa.”

Matamshi yake yanakuja siku moja tu kabla ya vijana wa Kenya kupanga kupiga hatua mitaani kwa lengo la kusukuma mageuzi na mapinduzi nchini Kenya.

Maandamano hayo yanakadiriwa kuzuka na makovu yake yanazidi kushuhudiwa na kuhisiwa kila kunapokucha.

Mpaka sasa, takriban zaidi ya wakenya hamsini hasa wengineo vijana na watoto wachanga wameripotiwa kufariki huku wengine wakitekwa nyara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved