KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi, Agosti 8.
Katika taarifa ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Kiambu, Nakuru, Kisumu, Nyeri, Embu, Meru na Kwale.
Katika kaunti ya Kiambu, maeneo ya Wangige na Mwimuto yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Eneo la Chuo Kikuu cha Egerton katika kaunti ya Nakuru litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maenelo ya mji wa Kibos na Kirdi katika kaunti ya Kisumu yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.
Katika kaunti ya Nyeri, maeneo ya Ihithe, Hubuini, na Kina yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Mugoya na Njakairi katika kaunti ya Embu yataathirika kati ya saa mbili unusu asubuhi na saa kumi unusu alasiri.
Sehemu za mji wa Meru na Thimangiri zitakosa katika kaunti ya Meru zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za mji wa Kwale na Kinango katika kauntiya Kwale pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.