KPLC yatangaza maeneo yatakayoathirika na kukatizwa kwa umeme leo, Ijumaa

Kampuni ya KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Agosti 9.

Muhtasari

•Kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Ijumaa, Agosti 9. 

Katika taarifa ya Ijumaa, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na  Kakamega, Homa Bay, na Murang'a.

Katika kaunti ya Kakamega, sehemu za eneo la Butere zitaathirika na kukatiuzwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu kadhaa za kaunti ya HomaBay zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Maragua, Ichagaki, Nginda, na Gachocho katika kaunti ya Murang'a zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.