KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumamosi, Agosti 10.
Katika taarifa ya Jumatatu jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Uasin Gishu, na Bungoma.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za barabara ya Mombasa Road na Southern Bypass zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Chemtech Factory, Jua Kali na Mo Gas katika kaunti ya Uasin Gishu yataathirika kati ya saa nne asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za mji wa Webuye, Pan Paper na Law Courts katika kaunti ya Bungoma zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa nane alasiri.