Gachaua kwa Wakisii: “Nyinyi shamba yenu ni kidogo, Affordable Housing itawajengea maghorofa”

“Sisi tuko hapa Gusiiland siku 3 kwa ajili ya maendeleo, na hasa mambo ya Affordable Housing, kwa sababu nyinyi Wakisii shamba yenu ni kidogo. Tunataka tuwajengee maghorofa, muishi ya ghorofa 14 huko juu mkiangalia dunia vile inakaa,” aliongeza.

Muhtasari

• "Tunataka tuwajengee maghorofa, muishi ya ghorofa 14 huko juu mkiangalia dunia vile inakaa,” aliongeza.

• Gachagua pia alimshukuru Osoro akimtaja kuwa mmoja wa wabunge wa chama tawala ambao ni wachapa kazi.

RIGATHI GACHAGUA
RIGATHI GACHAGUA
Image: FACEBOOK

Naibu wa rais Rigathii Gachagua kwa mara nyingine ameupigia debe mradi wa ujenzi wa nyumba nafuu nchini.

Akizungumza katika eneobunge la Mugirango Kusini kaunti ya Kisii wakati wa ziara ya siku tatu ya rais na naibu wake katika eneo pana la Gusii, Gachagua alianza kwa kuwashukuru wapiga kura wa eneo hilo kwa kumchagua mbunge Silvanus Osoro kwa tikiti ya chama cha UDA.

Gachagua alikiri kwamba tangu azaliwe ndio mara yake ya kwanza kufika katika eneo hilo.

“Leo nimefika hapa Etago, ukweli ni kwamba tangu nizaliwe sijafika hapa. Na tumekuja hapa tumemsindikiza rais kwa ajili ya mambo ya maendeleo. Tumekuja hapa kurudisha mkono kwa sababu hata nyinyi mlituunga mkono kwa kutuchaguliwa huyu Silvanus Osoro kwa chama cha UDA,” alisema.

Aliwarai viongozi wa eneo la Gusii kukumbatia mpango wa serikali wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika eneo hilo kwani jamii ya Abagusii wana mashamba madogo na hivyo itaifanya kuwa rahisi kuishi kaitka nyumba za maghorofa.

“Sisi tuko hapa Gusiiland siku 3 kwa ajili ya maendeleo, na hasa mambo ya Affordable Housing, kwa sababu nyinyi Wakisii shamba yenu ni kidogo. Tunataka tuwajengee maghorofa, muishi ya ghorofa 14 huko juu mkiangalia dunia vile inakaa,” aliongeza.

Gachagua pia alimshukuru Osoro akimtaja kuwa mmoja wa wabunge wa chama tawala ambao ni wachapa kazi.

“Pia nimekuja hapa kusema ahsante kwa huyu kijana Osoro. Huyu kijana katika wale wabunge tuko na wao, ni kijana ako na maono, na mimi na rais tukiangalia tunamlea, tunapanga yeye huko mbele atakuwa mtu wa maana. Kazi yenu ni kumuombea,” alisema.