• Kiongozi huyo wa chama cha NARC ameungwa mkono na aliyekuwa gavana wa kaunti ya Makueni Kivutha Kibwana.
• Itakuwa nafuu kwa jamii ya Akamba kuwa na waziri mwingine kando na waziri ya maswala ya kigeni Alfred Mutua.
Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Mutahi Ngunyi amemshauri rais William Ruto kumteua aliyekuwa gavana wa Kitui Charity Ngilu kama waziri ili kupunguza ushawishi wa kisiasa wa Kalonzo Musyoka Ukambani.
Kupitia ukurasa wake wa X, zamani ikijulikama kama Twitter, Ngunyi alisema kwamba Rais Ruto bado ana kazi ya kluifanya ili kusgawishi jamii ya Akamba kumuunga mkono, kwani bado wanamuunga mkono pakubwa kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka.
ngunyi alimtaka Ruto kuvunja nguvu za Kalonzo Ukambani kwa kumpa Ngilu kazi kama waziri wa Jinsia, wizara ambayo mpaka sasa haijapata waziri.
"Ili kumaliza ushawishi vwa Kalonzo, pengine rais Ruto abnafaa kumteua Charity Ngilu kama waziri wa jinsia. Hii itaziba pengo la Malonza na hivyo kumpa Ruto vigogo wawili wa siasa za Ukambani - Ngilu na Mutua. Wazo zuri?" Ngunyi alishauri.
Itakumbukwa Ngilu, ambaye alikuwa gavana wa Kitui kwa muhula mmoja tu ni mkereketwa wa jadi wa siasa za kinara wa Azimio, Raila Odinga.
Wakati huo huo, Alfred Mutua, ambaye alikuwa waziri wa utalii katika baraza la mawaziri lililovunjwa, alirudishwa hivi majuzi kama waziri wa leba.
Rais Ruto alilazimika kufanya mabadiliko hayo kwenye uongozi wake kufuatia msururu wa maandamano ya vijana wa Gen Z yaliyofanyika kwa zaidi ya wiki nne.
Wadhifa huo ambao bado ulisalia wazi katika wizara ya jinsia kufuatia kufutwa kazi kwa Aisha Jumwa ulitarajiwa kujazwa na Stella Soi ambaye hata hivyo jopo la kuwapiga msasa mawziri wateule likiongozwa na spika wa bunge Moses Wetang'ula lilimkataa katika wasilisho la ripoti bungeni wiki jana.