logo

NOW ON AIR

Listen in Live

KPLC yatangaza maeneo ambayo yatakosa umeme leo, Jumatatu

Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi na Homabay.

image
na Samuel Maina

Habari26 August 2024 - 03:59

Muhtasari


  • •KPLC imesema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
  • •Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi na Homabay.

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Agosti 26.. 

Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti mbili za Kenya yatakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni Nairobi na Homabay.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za eneo la Lower Kabete zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Baadhi ya sehemu za maeneo ya Woibero na Ojunge katika kaunti ya Homa Bay pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa tisa alasiri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved