KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumatano

Baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Muhtasari

•Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Dandora na barabara ya Kyuna zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Image: MAKTABA

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Agosti 28. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti nane za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Narok, Kakamega, Homabay, Migori, Kitui, Kilifi na Mombasa.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za mtaa wa Dandora na barabara ya Kyuna zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Rotian , Kisiriri, na Tipis katika kaunti ya Narok yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Soko la Lutaso katika kaunti ya Kakamega litakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika kaunti ya Homabay, maeneo ya Woibero na Ojunge yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za maeneo ya Sori na Otati katika kaunti ya Migori zitaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Kwa Kyenza, Kwa Mumo na Mutulu katika kaunti ya Kitui yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Eneo la Matsangoni katika kaunti ya Kilifi litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu ya kisiwa cha Mombasa katika kaunti ya Mombasa pia zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.