Raia wa Uganda akamatwa na polisi nchini Zimbabwe kwa kumiliki midoli ya kufanya mapenzi

Muhtasari

• Ssekamwa alikabiliwa na kesi ya kero ya jinai na kukiuka Sheria ya Udhibiti baada ya polisi kukuta kiungo cha kiume cha mpira kwenye begi lake.

• Hata hivyo, hakimu Isaac Chikura alimwachilia, akiamua kuwa kupatikana kwa toy hiyo ya ngono hakuathiri utulivu wa umma au kusababisha usumbufu wowote.

Mwanaume aliyekamatwa
Mwanaume aliyekamatwa
Image: Sagwe

Mamlaka nchini Zimbabwe zinaripotiwa kumfunga jela raia wa Uganda ambaye alikamatwa mapema mwezi huu akiwa na toy ya kufanya mapenzi.

Mshukiwa huyo anaarifiwa kukaa gerezani kwa zaidi ya wiki tatu kabla ya kuachiliwa huru kwa makosa yote.

Ssekamwa alikamatwa Agosti 2 nje ya nyumba ya kulala wageni huko Masvingo, jiji lililoko kilomita 292 kusini mwa Harare, pamoja na mtalii wa Czech Lucas Slavik, vyombo vya habari viliripoti.

Kukamatwa huko kulitokea wakati wa msako wa serikali dhidi ya wapinzani kabla ya mkutano wa kilele wa kanda, na kusababisha zaidi ya wanaharakati 200 wa upinzani na mashirika ya kiraia kuzuiliwa.

Ssekamwa alikabiliwa na kesi ya kero ya jinai na kukiuka Sheria ya Udhibiti baada ya polisi kukuta kiungo cha kiume cha mpira kwenye begi lake.

Hata hivyo, hakimu Isaac Chikura alimwachilia, akiamua kuwa kupatikana kwa toy hiyo ya ngono hakuathiri utulivu wa umma au kusababisha usumbufu wowote.

Hakimu alibainisha kuwa toy hiyo ya ngono ilikuwa kwenye begi la kibinafsi la Ssekamwa na hakukuwa na nia ya kuionyesha hadharani.

Wakili wa Ssekamwa, Knowledge Mabvuure wa Wanasheria wa Haki za Kibinadamu wa Zimbabwe (ZLHR), alithibitisha kuwa mteja wake kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa idara ya uhamiaji, akisubiri kufukuzwa na kurejeshwa nyumbani, Uganda.

"Changamoto tuliyonayo kwa sasa ni kwamba anahitaji kununua tiketi yake ya ndege ili kuondoka nchini, na simu yake ambayo anaweza kupata fedha zake bado inashikiliwa na polisi," alisema Mabvuure.