KPLC yatangaza maeneo ambako stima zitapotea leo, Jumatano

KPLC imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Septemba 4.

Muhtasari

•Kampuni ya KPLC ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

•Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Kakamega, Homabay, Nyamira, na Embu.

Kenya Power
Image: HISANI

KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya  (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Septemba 4. 

Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyiwa kwenye mitambo.

Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti sita za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Kakamega, Homabay, Nyamira, na Embu.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za Parklands na Muthaiga North Road zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za eneo la Chiga katika kaunti ya Kisumu zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa tisa alasiri.

Eneo la Lutaso katika kaunti ya Kakamega litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Maeneo ya Burlum, Seka, na Rambira katika kaunti ya Homabay pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Katika kaunti ya Nyamira, sehemu za mji wa Nyamira na Kebirigo zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.

Maeneo ya Kivaa na Masaku katika kaunti ya Embu pia yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.