logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nimechoshwa na uwongo wa Seneta Sakaja-Miguna amsuta Sakaja

Pia alidai kwamba alisikia haya kurudi darasani, hivyo basi hakukamilisha shahada yake.

image

Habari01 July 2022 - 14:10

Muhtasari


  • Wakili huyo akuptia kwenye akuanti yake ya twitter alihoji ni kwa nini Sakaja alikuwa akilaumu shahada yake ya UoN ambayo haijakamilika juu ya umaskini

Wakili Miguna Miguna amemsuta Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja kuhusu kusukuma na kuvuta shahada yake.

Wakili huyo akuptia kwenye akuanti yake ya twitter alihoji ni kwa nini Sakaja alikuwa akilaumu shahada yake ya UoN ambayo haijakamilika juu ya umaskini.

"Nimechoshwa na uwongo wa Sakaja. Alikuwa ameeleza hadharani jinsi alivyokuwa mfanyabiashara milionea akiwa na gari la Mercedes Benz alipokuwa UoN. Jinsi alivyokulia katika kaya ya Atwoli (bosi wa COTU)," aliandika.

Matamshi yake Miguna yanajiri saa chache baada ya seneta huyo kudai kwamba hakumaliza masomo ya shahada yake kwa sababu hakuwa na karo ya shule.

Pia alidai kwamba alisikia haya kurudi darasani, hivyo basi hakukamilisha shahada yake.

"Alisema alikuwa na Digrii ya Sayansi ya Aktuari. Kwa nini sasa analia juu ya umaskini?" Miguna aliuliza.

Huko nyuma, Sakaja aliwahi kudai kuwa alihitimu shahada ya kwanza ya Sayansi ya Actuarial kutoka UoN, lakini chuo kikuu kilikanusha madai hayo.

Walisema ingawa Seneta huyo alikuwa mwanafunzi katika chuo hicho, hakuwahi kumaliza masomo yake.

Mnamo 2021, akizungumza na mtangazaji wa Churchill Show Daniel Ndambuki, Sakaja alifichua kwamba alinunua gari lake la kwanza, Mercedes Benz, alipokuwa chuo kikuu.

Alisema ilimgharimu Sh500,000.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved