logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kasarani: Matukio katika picha, hafla ya kuapishwa kwa rais Ruto

Kiongozi huyo alitangazwa mshindi mnamo Agosti 15 na tume ya IEBC na ushindi wake ukaidhinishwa na jopo la majaji saba wa mahakama ya upeo mnamo Septemba 5.

image
na Radio Jambo

Uchaguzi13 September 2022 - 04:50

Muhtasari

• Ruto anatarajiwa kuapishwa kama rais wa tano akichukua hatamu kutoka kwa rais anayeondoka, Uhuru Kenyatta.

Matukio katika picha kutoka Kasarani kuapishwa kwa rais Ruto

Jumanne Septemba 13 ni siku ya kihistoria nchini Kenya taifa likitarajia kushuhudia kuapishwa kwa rais wake wa tano, William Ruto.

Ruto anaingia katika vitabu vya historia kama rais wa kwanza kuchaguliwa baada ya kufanya jaribio katika wadhfa huo kwa mara ya kwanza kabisa.

Vile vile Ruto ndiye naibu wa kwanza wa rais kuchaguliwa kama rais, si tu chini ya katiba mpya ya mwaka 2010 bali pia hata katiba ya awali tangu uhuru, hakujawahi tokea naibu au makamu wa rais kuwania na kuchaguliwa kwa mara ya kwanza.

Kiongozi huyo alitangazwa mshindi mnamo Agosti 15 na tume ya IEBC na ushindi wake ukaidhinishwa na jopo la majaji saba wa mahakama ya upeo mnamo Septemba 5.

Hapa tunakuandalia baadhi ya matukio katika picha jinsi shughuli ya kuapishwa kwake inaendelea katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani, ambapo inaarifiwa wakenya wengi walifika pale tangu alfajiri ya jogoo la kwanza tayari kushuhudia hafla hiyo ya kihistoria.

Matukio katika picha Kasarani kuapishwa kwa Ruto
Matukio katika picha Kasarani kuapishwa kwa rais Ruto

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7

logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved