Usiku wa Jumatatu wezi wane waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliingia katika duk moja na kuiba mikate pamoja na kima cha shilingi elfu 21.
Kulingana na jarida la Nation, tukio hilo lilifanyika katika daraja la Manguo, karibu na Clay city huko Kasarani, Kaunti ya Nairobi, kulingana na ripoti ya polisi iliyoonwa.
“Yote yalianza wakati gari la Hyundai lililokuwa likiendeshwa na Bw Nicholas Mutie, 38 na Bw Faruk Ongaki, 22 liliposimamishwa na watu wanaoshukiwa kuwa majambazi,” Nation waliripoti.
Genge hilo la wezi wenye silaha walisimamisha gari liilokuwa limesheheni kreti 281 za mikate kabla ya kuagiza dereva na utingo wake kuwapatia simu zao, amri ambayo walitii kabla ya kuanza kufanya wizi wa mikate kabla pia na kuiba mafuta kutoka tenki la lori hilo.
“Washukiwa hao pia walibomoa kifaa cha kufuatilia na kuchomoa mafuta yote na kupakia mkate huo kwenye gari ambalo nambari yake ya usajili haikunaswa. Gari hilo lililokuwa limebeba mikate hiyo lilivutwa hadi katika Kituo cha Polisi cha Kasarani,” Nation walisema.
Taarifa hizi zinakuja sambamba na taarifa zingine zilizoripotiwa pia kutoka eneo hilo la Kasarani baada ya mwanaume mweney umri wa miaka 29 kupatikana na simu aina ya Iphone zaidi ya 265 na pia simu za Android zipatazo 10.
Taarifa za polisi zilisema kwamab jamaa huyo alishikilia na alikuwa ametarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne Novemba 22.
Simu hizo zilikisiwa kuwa za wahanga wa ujambazi na wizi wa kimabavu ambao umekuwa ukitokea kwa wiki mbili zilizopita jijini Nairobi.