Mike Sonko amejitokeza kumjibu Robert Alai baada ya kumwambia kuwa alikuwa akijigamba na pesa zake mtandaoni.
Kashfa za Alai zilijiri baada ya Sonko kusambaza video kwenye mitandao ya kijamii inayoonyesha mamia ya dola zikiwa zimerundikwa kwenye sanduku nyumbani kwake.
Alai alimwambia kuwa anaweza kuwa tajiri lakini kiakili ni maskini.
Sonko hakupenda kile Alai alisema na kama kawaida alimjibu. Sonko alimkumbusha Alai kwamba walikuwa marafiki wazuri na atakumbuka hilo daima.
Kisha akamwambia kwamba ikiwa atakufa mapema kuliko yeye atahakikisha anazikwa kama mfalme. Aliahidi kujenga nyumba ya kisasa nyumbani kwake kijijini kabla ya kuzikwa.
"Na bado ujue bado naweza kutoka kwa mtu yeyote ukiwemo wewe mwenyewe kwa vile ulikuwa rafiki yangu Godforbid akikuchukua mbele yangu, nitahakikisha unazikwa kama mfalme. Pamoja na kamati yako ya mazishi tutauhifadhi mwili wako chumba cha kuhifadhia maiti kwa wiki 3 zaidi huku nikikujengea nyumba ya kisasa kwenye shagi zako ambapo utapumzishwa." Sonko alijibu Alai.
Ujumbe wa Alai ulisoma;
"Ukweli kwamba unaweza kutumia kamera na kuonyesha sehemu ya pesa haukufanyi uwe tajiri.Unaweza kuwa na pesa nyingi ukiwa ghorofani, wewe ni maskini wa ki akili.Jamani, tafuteni maarifa na hekima. Gig piny bura olyo.Usiwahi kutafuta uthibitisho kutoka kwa watumiaji wa mtandao,"Alai alisema
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakitoa hisia mseto baada ya gavana huyo wa zamani wa kaunti ya Nairobi kuonekana katika video akijigamba kuhusu noti za pesa za Kenya na dola za Marekani alizofadhi nyumbani kwake.
"Ati sina pesa kwa sababu sisaidi watoto... Nani ali kwambia sina pesa!?" Sonko kwa hasira tele alimfokea mtu huyo ambaye hakutajwa jina ambaye bila shaka alikuwa amemkera sana hadi kwenye koo.
"Sina pesa ya kusaidia watoto. Hii pesa ni ya kuharibu mabibi wangu!" mwanasiasa huyo asiyepungukiwa na drama alisema huku akionyesha mamilioni ya pesa ambazo alisema ni za kujaza mafuta kwenye magari yake.
Kwa maneno yake mwenyewe, gavana huyo wa zamani alidai kuwa alikuwa akihifadhi zaidi ya milioni 30 kwenye nyumba.
Tangu video hiyo kuchapishwa mitandaoni, Wakenya wamekuwa wakitoa maoni mseto, baadhi wakimshambulia huku wengine wakimtetea.
Bi Sandra ambaye bila shaka hakufurahishwa na mashambulizi dhidi ya baba yake amewaomba Wakenya kumuelewa huku akibainisha kwamba ni kawaida kwa mtu yeyote kupandwa na hasira katika nyakati fulani.
"Jamani naomba muache kumshambulia baba yangu kwenye hiyo video. Kila mtu anakasirika na kama ungekuwa wewe kwenye nafasi hiyo ungepinduka zaidi," Sandra alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.