logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wanandoa wa Kakamega washtuka baada ya kugundua mimba licha ya mume kufanyiwa vasektomi

Beryl aliweka wazi kuwa ujauzito wake haukuleta shida na mumewe kwani wanaaminiana sana.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri18 May 2023 - 09:34

Muhtasari


•Medgclay ,36, alifanyiwa upasuaji wa masaa mawili mnamo Julai 12, mwaka jana lakini miezi michache baadaye mkewe Beryl, 33, alithibitishwa kuwa mjamzito.

•Wanandoa hao walisema mwanzoni walidhani Beryl alikuwa amechelewa kupata hedhi kwa kuwa hawakufikiria kuwa anaweza kuwa mjamzito.

Wanandoa kutoka kaunti ya Kakamega bado wako katika mshtuko baada ya mwanamke kupata ujauzito licha ya mumewe kufanyiwa upasuaji wa kupanga uzazi (Vasektomi).

Medgclay ,36, alifanyiwa upasuaji wa masaa mawili mnamo Julai 12, mwaka jana lakini miezi michache baadaye mkewe Beryl, 33, alithibitishwa kuwa mjamzito.

Wakizungumza na Mwananchi Digital, wanandoa hao waliweka wazi kwamba walifuata miongozo yote iliyotolewa na daktari baada ya upasuaji.

“Daktari aliniambia kwamba tungekuwa salama baada ya kumwaga mbegu za kiume mara 20 ama baada ya miezi mitatu. Kwa hivyo tulikuwa salama baada ya mwezi wa saba, wa nane na wa tisa,” Medgclay alisema.

Medgclay alisema kuwa hata hivyo alianza kuwa na mashaka mwezi Novemba kwani mkewe alikuwa bado hajapata hedhi miezi kadhaa.

Wanandoa hao walisema mwanzoni walidhani Beryl alikuwa amechelewa kupata hedhi kwa kuwa hawakufikiria kuwa anaweza kuwa mjamzito.

“Ilipofika Desemba tulisema imeenda miezi mitatu karibu minne. Tulipoenda kupima tukajua ako na ujauzito. Ilikuwa mshtuko kwetu kwa sababu hatukuwa tunatarajia,” alisema.

Alisema pia walikuwa na wasiwasi kwa sababu Beryl alikuwa amejifungua mtoto wao wa tatu kupitia njia ya upasuaji miezi michache tu iliyokuwa imepita. Madaktari hata hivyo waliwathibitishia kuwa hali ni ya kawaida na walitakiwa kusubiri hadi mtoto atakapozaliwa baadaye mwezi huu ili kujua nini kilienda vibaya.

Beryl aliweka wazi kuwa ujauzito wake haukuleta shida na mumewe kwani wanaaminiana sana. Alisema kuwa mwanzoni alikana baada ya kuanza kushuku ni mjamzito na alikuwa na alihofia kuibua mada hiyo na mumewe.

Alithibitisha kuwa yeye na mume wake walikuwa na mazungumzo na wakafikia makubaliano kabla ya mchakato wa Vasektomi. Alisema kwamba mwanzoni alikuwa na hofu hiyo

“Alipozungumza kuhusu hayo niliuliza itakuwaje. Nilishangaa ikiwa inaweza kuathiri maisha yetu ya mapenzi. Niligundua kuwa haiathiri, kwa kweli imekuwa bora, " alisema.

Alisema kwamba walifurahi sana kuhusu utaratibu huo na akafichua kwamba mume wake alipona baada ya wiki moja.

Alibainisha kwamba alitumia vidonge vya kupanga uzazi kwa takriban miezi 3 kabla ya muda uliowekwa na daktari ili kuwa salama kwa mapenzi bila kutumia mbinu zingine za kupanga uzazi kufika.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved