Katika ulimwengu ambapo nchi nyingi hazikuruhusu kuzungumza waziwazi kuhusu ngono, Uswidi imekuwa nchi ya kwanza ulimwenguni kutangaza rasmi kushiriki mapenzi kama mchezo na pia iko tayari kuandaa shindano lake la kwanza kabisa la kufanya mapenzi, jarida la Times of India linaripoti.
Kulingana na ripoti hiyo ambapo iligonga vichwa vya habari katika mataifa mengi wikendi, Washiriki watashiriki katika vipindi vya ngono ambavyo vinaweza kwenda hadi saa sita kila siku.
Jopo la majaji litaamua washindi wa shindano la ngono huku watazamaji pia wataathiri maamuzi ya mwisho.
Likitajwa kwa jina Mashindano ya Ngono ya Ulaya, shindano hilo litaanza wiki hii, Juni 8, na kuendeshwa kwa muda wa wiki sita huku washiriki wakijihusisha na ngono kutoka dakika 45 hadi saa 1 kila siku, kulingana na muda wa mechi zao.
Kando na kushawishi uamuzi, hadhira pia itagundua vipengele kadhaa vya shughuli ya kufanya mapenzi.
Uamuzi wa mwisho kuhusu washindi utafikiwa baada ya kuzingatia vipengele kama vile kemia kati ya wanandoa hao, ujuzi kuhusu ngono na kiwango cha uvumilivu.
Kulingana na jarida hilo, watu Zaidi ya 20 tayari wameshatuma maombi yao wakitaka kushirikishwa katika mchezo huo na mshindi atapatikana kupitia kura za watazamaji na pia majaji watatu.
Uwiano wa wanandoa, uelewa wao kuhusu mchezo wa kufanya mapenzi, kiwango chao cha uvumilivu, na vipengele vingine muhimu vya ngono vyote vitazingatiwa wakati wa kuamua ni nani ataibuka mshindi.
Mkuu wa Shirikisho la Ngono la Uswidi, Dragan Bratych, alisema anatumai kuwa siku moja mchezo wa ngono utazingatiwa kama mchezo ulimwenguni.
Alisisitiza umuhimu wa elimu na uwezekano kwamba kushiriki ngono kunaweza kuboresha afya ya mtu kimwili na kiakili.
