logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DP Gachagua azungumzia picha iliyoenea akimkaribisha Raila Odinga KICC

"Nilimkaribisha kwa heshima kwa sababu yeye ni mzee wetu amekuja, tumemualika."

image
na Radio Jambo

Habari09 September 2023 - 10:15

Muhtasari


• Gachagua alisema kuwa baada ya Odinga kutaka kufanya jaribio la kwenda kwa marais wengine, kila mtu aliuliza “huyu ni rais wa wapi?”

Raila na Gachagua

Naibu wa rais Rigathi Gachagua kwa mara ya kwanza amezungumzia kilichojiri katika picha ambayo imeenezwa sana mitandaoni ikimuonesha yeye akimkaribisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika ukumbi wa KICC katika kilele cha mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa mapema wiki iliyopita.

Akizungumza Ijumaa, Gachagua alisema kwamba kilichomfanya kumkaribisha Odinga ni kwa sababu wanamheshimu kama mzee wa taifa.

Hata hivyo, Gachagua aiwavunja watu mbavu kwa kuibua madai kwamba baada ya kumkaribisha, Odinga alitaka kukimbia kwenda kwenye upande waliokuwa wanaketi marais wa mataifa mbali mbali badala ya kuketi katka sehemu aliyokuwa ametengewa mbali na marais waliochaguliwa.

Gachagua alisema kuwa Odinga alikuwa anataka kukosa adabu kwani ilikuwa ni kuvunja itifaki kwenda kwa marais waliochaguliwa hali ya kuwa yeye hajachaguliwa na wananchi kama rais.

“Juzi nimemkaribisha pale KICC, si mliona. Nilimkaribisha kwa heshima kwa sababu yeye ni mzee wetu amekuja, tumemualika, sasa kuliko aende aketi kwa kiti chake, alitaka kwenda kuketi kwa marais ambao wamechaguliwa. Na huyu mtu amechaguliwa na mtu kweli? Ile nyumba hata Kipchumba [Murkomen] huyu ni waziri hawezi ingia. Ni marais tupu wameketi. Marais wamejaa pale, eti anataka kuingia pale aketi na marais,” Gachagua alimshambulia Odinga.

Gachagua alisema kuwa baada ya Odinga kutaka kufanya jaribio la kwenda kwa marais wengine, kila mtu aliuliza “huyu ni rais wa wapi?”

“Pale kwenye ukumbu tulimpa kiti cha heshima, hata alikuwa nambari 4 kutoka kwangu. Ameketi pale kama mzee anasikiliza maneno, akikaakaa usingizi ukizidi anang’orota kidogo muda unaenda. Hakuna shinda, huyo ni mzee wetu na nilimuambia tunataka tumchunge,” Gachagua aliongeza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved