logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wajackoyah ampigia debe Eric Omondi kushinda Lang'ata, amtaka Jalang'o kujiuzulu

“Kuna watu pale wanataka kujua eti nani Baba ataenda kuuna mkono." - Wajackoyah.

image
na Radio Jambo

Habari21 September 2023 - 06:56

Muhtasari


• Alisisitiza kwamba watu hao hawatapata nafasi hata kidogo ya kuungwa mkono na Odinga wakati wanafanya mambo ya kukipiga chama cha ODM vita kinyemela.

Wajackoyah na Omondi

Aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka jana kupitia tikiti ya chama cha Roots, wakii msomi George Wajackoyah anadai kuna watu ambao wanamzunguka kinara wa ODM Raila Odinga ambao wamenzisha mchakato wa chini kwa chini kupanga jinsi watakavyomrithi kisiasa akiwa hai.

Akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni, Wajackoyah alisema kwamba muda si mrefu wataweka wazi majina ya watu hao ambao wanajinyenyekeza karibu na Odinga ili kupata ushawishi wa kisiasa kwa kumtumia kama ngazi ya kukwea.

“Akili ya Baba [Raila Odinga] ni safi bado lakini kuna watu wanaomzunguka na wanamtumia kama ngazi, na tayari tumegundua wanapanga kumrithi Baba kabla hata hajafa,” Wajackoyah alisema.

Alisisitiza kwamba watu hao hawatapata nafasi hata kidogo ya kuungwa mkono na Odinga wakati wanafanya mambo ya kukipiga chama cha ODM vita kinyemela.

Wajackoyah alimpigia debe mwanaharakati Eric Omondi kama mtu ambaye anaweza kumsaidia Odinga kuliko hata wanasiasa wengine ambao wanachokiangazia sasa hivi ni kumrithi Odinga.

“Kuna watu pale wanataka kujua eti nani Baba ataenda kuuna mkono. Wako pale tu kwa sababu wanataka waingie kwa mguu wa Baba. Unarithi aje ODM? Huyo ndio mama wa Baba ukiachia mbali Mama Ida. Na tutawaweka wazi wale walaghai ambao wameketi karibu na Baba, muda wenu umekwisha, sasa hivi tuna vijana kama Eric Omondi hapa ambaye anaweza kumsaidia Baba. Na mimi nitamuunga mkono Eric Omondi Lang’ata,” Wajackoyah alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved