Migori: Vita kati ya mrembo wa miaka 24 na baba mkwe wa miaka 70 yaishia pabaya

Mzee huyo alimshambulia mke wa kijana wake kwa panga kabla ya mwanamke huyo kumzidia na kumpokonya ile panga na kumcharanga maeneo ya kichwa vibaya mno.

Muhtasari

• Mzee huyo bado amelazwa hospitalini kufuatia vita na mkwewe. Mamlaka imetoa wito kwa wenyeji kutafuta njia bora za kushughulikia mizozo.

Mwanamke mjamzito apatikana amedungwa visu mgongoni
Mwanamke mjamzito apatikana amedungwa visu mgongoni
Image: Maktaba//The Star

Vita kati ya mwanamke wa miaka 24 na baba mkwe wake anayekisiwa kuwa katika miaka yake ya 70s iliishioa pabaya baada ya wawili hao kushambuliana kwa panga na kujeruhiana vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Citizen, mwanamke huyo aliwachukua ng’ombe wake kuwalisha katika kiwanja cha nyasi ambacho mzee huyo alijitokza na kusema kwamba ni kiwanja chake na kumtaka mke wa mwanawe kuwaondoa ng’ombe.

Hapo ndipo walianza kubiashana kabla ya baba mkwe kumshambulia kwa panga mke wa kijana wake.

Katika hali ya kujibu mipigo, mwanamke huyo naye alimzidia mzee nguvu na kumpokonya panga ile kabla ya kuitumia kumjeruhi vibaya katika maeneo ya kichwa, kupeleka yeye kukimbizwa hospitalini akiwa anatiririkwa na damu.

Chifu wa Kajulu II, Charles Onindo aliambia Citizen kuwa wawili hao walipata majeraha makubwa kufuatia kisa hicho.

"Nilikimbilia eneo la Onge’nga baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi," Onindo alisema.

"Suala hilo bado linachunguzwa, na baada ya hapo hatua muhimu zitachukuliwa," mkuu huyo aliongeza.

Mzee huyo bado amelazwa hospitalini kufuatia vita na mkwewe. Mamlaka imetoa wito kwa wenyeji kutafuta njia bora za kushughulikia mizozo.

"Nitaongoza mkutano na familia pindi mzee huyo atakapoachiliwa katika juhudi za kuwapatanisha wawili hao," Onindo alibainisha.