Tukio hilo limelaaniwa na watu wengi mitandaoni

Dunia simama nishuke! Tazama video, mhubiri akiwataka waumini wa kike kuvua chupi na kuwanyoa nyeti zao+Video

Sio mara ya kwanza kwa video kama hii ya kushangaza hasa kanisani kujitokeza

Muhtasari

 

  •  Video hiyo imewashangaza watu wengi 
  • Mhubiri anaahidi miujiza kwa waliofanyiwa kitendo hicho 

 

Kwa kweli walimwengu tumevuka mipaka na hasa katika kulitumia jina la mwenyezi Mungu vibaya. Kumekuwa na visa vya watu kufanya vitendo vya kutisha na ajabu kwa kulitumia jna la mola kumbe bado mengi yanakuja.

 Video moja inayosambazwa mitandaoni imeomunyesha mhuburi mmoja nchini Ghana akiwaita waumini wake wa kike kanisani na kisha kuwaagiza watoe chupi zao na kuwanyoa sehemu zao nyeti! Mchana peupe huku waumini wengine wakionekana kushangilia .

Wololo! Yaani ulimwengu umefika hapa?Mhubiri awatoa chupi waumini wa kike na kuwanyoa kanisani !

 Katika  video hiyo, kuna mwanamume wa pili ambaye anamsaidia mhubiri huyo katika  kazi hiyo. Wanawake wa umri wa makamu na umri mdogo wanaonekana wakikimbia kwenda jukwaani ili kunyolewa  nywele za  siri  na ‘mtu huyo wa mungu’

 

Pasta huyo kwanza anachukua muda kuwaombea  waumini hao  na anasikiza akiongea lugha ya kwao kisha kuwashika sehemu zao za siri na kuanza kuwatoa chupi na baadaye kuwanyoa.

 Watu wengi katika mitandao ya kijamii wamekea sana kitendo hicho.

Kwa kweli dunia yaelekea wapi?

(Mhariri Davis Ojiambo)