Ghost Mulee ahusika katika ajali ya barabarani

Muhtasari

• Alikuwa njiani akielekea kazini mwendo wa saa kumi na moja asubuhi

• Alikimbizwa hospitalini na hali yake ni thabiti 

• Gari lake liligongwa na matatu katika upande wa dereva 

Gari la Ghost Mulei punde tu baada ya ajali siku ya Ijumaa
Gari la Ghost Mulei punde tu baada ya ajali siku ya Ijumaa

Mtangazaji wa Radio Jambo Jacob Ghost Mulee amehusika katika ajali ya barabarani mapema siku ya Ijumaa alipokuwa anaelekea kazini.

Mulee alikimbizwa katika hospitali ya Agha Khan punde tu baada ya ajali hiyo kutokea na yuko katika hali thabiti.

Gari la mtangazaji huyo wa kipindi cha ‘Gidi na Ghost asubuhi' liligongwa kwa upande wa dereva na matatu mwendo wa saa saa kumi na moja unusu.

Ghost Mulee
Ghost Mulee
 
 
 
 

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Brookside kwenye barabara kuu ya Waiyaki, wakati gari lake lilipogongwa  na matatu ya KMO iliyokuwa ikiendeshwa kwa kasi kuelekea mjini Nairobi kutoka eneo la Kangemi.

Gari la Ghost ambalo limeharibika vibaya limevutwa hadi kituo cha polisi cha Spring Valley.

Alikimbizwa hospitalini na msanii Jalang'o ambaye amesema alikuwa anafanyiwa vipimo kuthibitisha ikiwa alipata majeraha zaidi.

Meza ya habari ya Radio Jambo inamuombea Ghost afueni ya haraka.