logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu 10 wafariki huku 780 wakipatikana na Corona

Leo watu 552 wamepona Corona na kufikisha 53,526 idadi ya watu waliopona ugonjwa huo .

image
na Radio Jambo

Habari26 November 2020 - 12:18

Muhtasari


 

  •  Leo watu 552 wamepona Corona na kufikisha 53,526 idadi ya watu waliopona ugonjwa huo .
  • Wagonjwa 1,232 wamelazwa katika hospitali mbali mbali  kote nchini ilhali 7,295 wapo chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani

 

kagwe

Watu 780 wamepatikana na virusi vya Corona  baada ya sampuli 6,158 kupimw katika saa 24 zilizopita  na kufikisha 80,102 jumla ya visa vya ugonjwa huo nchini huku idadi ya sampuli zilzipimwa ikifika 861,561 .kutoka visa hivyo 754 ni wakenya ilhali 26 ni raia wa kigeni .460 ni wanaume huku wanawake wakiwa 320 .Mgonjwa wa  umri wa chini ni mtoto wa mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu ana miaka 94 .

 Leo watu 552 wamepona Corona na kufikisha 53,526 idadi ya watu waliopona ugonjwa huo .

Hata hivyo watu 10 wameaga dunia na kufikisha 1,427 watu walioangamizwa na Corona kufikia sasa .

 Wagonjwa 1,232 wamelazwa katika hospitali mbali mbali  kote nchini ilhali 7,295 wapo chini ya mpango wa kutunzwa nyumbani .wagonjwa 57 wapo ICU huku 24 wakiwa katika kitengo cha HDU

  


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved