MCK yafuta uanachama wa mwanahabari mmoja kwa utovu

Muhtasari

• MCK ilisema uanachama wa Dennis Kipyego umesitishwa kwa muda kwa kwenda kinyume na Kanuni na Maadili ya Uandishi.

Baraza la Vyombo vya Habari nchini Kenya (MCK) limefutilia mbali uanachama wa mwandishi wa habari kwa kutovu wa nidihamu.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya Ijumaa, MCK ilisema uanachama wa Dennis Kipyego umesitishwa kwa muda kwa kwenda kinyume na Kanuni na Maadili ya Uandishi wa Habari.

"... Uanachama wa Kipyego MCK015913 umesitishwa kwa utovu wa maadili. Hii ni kwa sababu ya kukiuka kanuni na maadili ..," ilisema taarifa hiyo.

Kulingana na mtandao wa linkedIn, Kipyego ni mwandishi wa habari wa kujitegemea na Media Max.

MCK ilisema haitachukua jukumu la shughuli zozote kati ya Kipyego na umma kwa sababu ya uanachama wake wa MCK.

Baraza la vyombo vya habari liliendelea kusema kwamba limeweka utaratibu anuwai kusaidia kuthibitisha hadhi ya mwandishi wa habari, kuripoti kesi za ukiukaji dhidi ya waandishi wa habari, matamshi ya chuki na habari bandia.

Sheria ya Vyombo vya Habari 2013 inasimamia mienendo na utendakazi wa sekta ya habari nchini.