Ajali! kaunti ya kilifi yaomboleza vifo vya wafanyikazi sita

Muhtasari

• Gavana Amason Kingi alithibitisha kupoteza wafanyikazi wake  akisema wengi waliofariki ni wa idara ya ukusanyaji pesa.

• Ajali hiyo  ilihusisha basi la kampuni ya Muhsin Bus  na basi la kampuni ya Sabaki Shuttle.

Image: ALPHONSE GARI

Serikali ya kaunti ya Kilifi inaomboleza vifo vya wafanyikazi wake sita.

Sita hao walikuwa miongoni mwa watu 15 waliofariki katika ajali mbaya ya barabarani siku ya Jumatano katika eneo la Kwamkikuyu kwenye barabara kuu ya Malindi Mombasa.

Maafisa wa kaunti sita pamoja na wengine ambao walinusurika walikuwa safarini wakielekea kazini na walikuwa wameabiri basi ya kampuni ya Sabaki kutoka eneo la Marereni ajali hiyo ilipotokea.

 

Gavana wa Kilifi Amason Kingi alithibitisha kupoteza wafanyikazi wake.

“kwa kawaida wao hutumia basi ndogo kusafiri kutoka Malindi ambapo wanakaa hadi Kilifi wanako fanyia kazi,” Kigi alisema alipozuru eneo la ajali.

Alisema wengi waliofariki ni wa idara ya ukusanyaji pesa.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kwamkikuyu na ilihusisha basi la kampuni ya Muhsin Bus lililokuwa safarini kwenda Garissa kutoka Mombasa na basi la kampuni ya Sabaki Shuttle lililokuwa likielekea Merereni.

Madereva wote wawili walifariki papo hapo.