Msichana wa miaka 15 akamatwa kwa kuavya na kutupa vijusi chooni

Muhtasari

• Mkurugenzi wa DCI George Kinoti alisema wapelelezi waliokoa kijusi kimoja katika hali mbaya baada ya kutupwa katika shimo cha la choo.

• Watoto hao walikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Bartabwa huko Kabartonjo, ambapo mmoja alitangazwa kufariki

Pingu
Image: Radio Jambo

Msichana wa miaka 15 amekamatwa baada ya kuavya mimba huko Kabartonjo katika kaunti ya Baringo.

Mkurugenzi wa DCI George Kinoti alisema wapelelezi waliokoa kijusi kimoja katika hali mbaya baada ya kutupwa katika shimo cha la choo.

Maafisa ambao walikuwa wamepata ripoti kutoka kwa majirani walifanya haraka kubomoa choo na kuokoa kitoto hicho.

"... walipongia ndani waligundua kwamba kulikuwa na vijusi viwili vilivyokuwa vimezama ndani ya kinyesi cha binadamu," Kinoti alisema.

Watoto hao walikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Bartabwa huko Kabartonjo, ambapo mmoja alitangazwa kufariki, wa pili alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Baringo kwa matibabu maalum.

Mtuhumiwa atashughulikiwa kisheria kulingana na makosa yake.

Kulingana na katiba, kila mtu ana haki ya kuishi na kwamba maisha ya mtu huanza wakati wa kutungwa.