KRA yafunga akaunti za vyuo kikuu vya Nairobi na Kenyatta

Muhtasari

• Naibu Chansela wa UON Stephen Kiama alikiri kwamba chuo hicho kinadeni la KRA la 7 bilioni na kufichua taasisi hiyo inakumbwa na matatizo ya ko katika shida ya kifedha.

uon-law-campus
uon-law-campus

Mamlaka ya Mapato nchini (KRA) imezifunga kwa muda akaunti za benki za vyuo vikuu viwili nchini kwa kile sasa kinatishia kulemaza elimu ya juu nchini Kenya.

KRA izifunga akaunti za Chuo Kikuu cha Nairobi na Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa nia ya kupata mabilioni ya pesa yanayodaiwa na taasisi hizo kutokana na ushuru ambao haujalipwa.

Taasisi hizo mbili hazijawasilisha makato ya kodi za kisheria – ushuru unaotozwa kwa mishahara – PAYE, kiasi ambacho sasa kimetimia mabioni ya pesa.

 

Gazeti la Star limebaini kuwa KRA imeambatanisha akaunti za benki za Chuo Kikuu cha Nairobi yenye kima shilingi milioni 450, na kuweka mipango ya elimu ya chuo kikuu katika hatari.

Haikufahamika mara moja jinsi wafanyikazi wa vyuo vikuu watakavyolipwa, na kuongeza hofu ya hatua za migomo.

Akaunti zote za benki za Chuo Kikuu cha Kenyatta pia zilifungwa.

"Kinachotokea ni cha kusikitisha. Ni kama serikali inapigana na serikali," duru zilisema.

Siku ya Jumapili, Naibu chansela wa chuo Kikuu cha Nairobi Prof Stephen Kiama na mwenzake wa KU Prof Paul Wainaina walikiri taasisi hizo zinadaiwa pesa nyingi na KRA lakini walikanusha akaunti zao zimefungwa.

“Akaunti za UoN hazijagandishwa. Tumefanya mipango na KRA juu ya jinsi ya kukabiliana na PAYE kusonga mbele, "Prof Kiama alisema.

"Chuo Kikuu cha Nairobi hakiathiriwi kwa sababu tulikuwa na mazungumzo mazuri na maafisa wa KRA na chuo kilijitolea kufanya juhudi kundelelea kulipa," akaongeza.

 

Kiama alikiri kwamba chuo hicho kinadeni la KRA la 7 bilioni na kufichua taasisi hiyo inakumbwa na matatizo ya ko katika shida ya kifedha.