VITA VYA PALESTINA

Israeli yalipua mnara unazo ofisi za Al jazeera Gaza

israeli ilikuwa imepeana onyo kuwa ingelipua mnara wa Al Jalaa ulikuwa na makao ya shirika la kijeshi la Hamas na ofisi za nyumba nyingi za Habari za kimataifa ikiwemo Al Jazeera.

Muhtasari

•Wanajeshi wa Israeli walikuwa wamepeana onyo

•Mnara wa Al Jalaa ulikuwa unatumika na kikundi cha Hamas kutekeleza shughuli za kejeshi

Mashambulizi ya mnara wa Al Jalaa
Mashambulizi ya mnara wa Al Jalaa
Image: HISANI

Wanajeshi wa Isreali wamelishambulia kwa bomu na kubomoa mnara wa Al Jalaa ambao una maofisi ya nyumba za habari za kimataifa ikiwemo Al Jazeera na zingine.

Mnara huo ambao pia unatumika kuhifadhi mali ya  kijeshi ya shirika la Hamas limelipuliwa muda mfupi baada ya kutoa onyo kuwa wangelipua  mnara huo.

Hamas ambacho ni kikundi cha kijeshi tokea Palestina kinatawala Gaza kimekuwa lengo la wanajeshi hao wa Israeli kwa muda.

Kupitia akaunti yao ya Twitter, wanajeshi wa Israeli wamesema kuwa shirika la Hamas limekuwa likitumia makazi ya watu kwa shughuli za kijeshi kama kukusanya habari, kupanga shambulio,kutoa amri kudhibiti nakuwasiliana.

“Hamas wakitumia minara kutekeleza shughuli za kijeshoi basi  ni kinyume na sheria na mnara huo unakuwa lengo la shambulio la wanajeshi.” Israeli imetangaza.

Wanajeshi hao wametangaza kuwa wamekuwa wakilipua majumba kama hayo ila wanawapatia watu ilani ya kuhama kabla ya kutekeleza shambulio.

“Majumba yote tuliyobomoa yamekuwa yakitumia kwa shughuli za kijeshi.” Wanajeshi hao wamedai.