POLISI MUUAJI

Polisi akamatwa kwa tuhuma za mauaji Rongai

Konstabu Okimaru amepatikana kuwa mshukiwa mkuu kwenye mauji ya kondakta wa Rongai.

Muhtasari

•Mungai, George na Njenga walikuwa wamekamatwa kwa kukiuka sheria za curfew

•Marehemu alikufa kutokana na majeraha aliyopata kifuani baada ya kushambuliwa.

151
151

Askari mmoja anayefanya kazi katika kituo cha polisi cha Dabel mjini Moyale amekamatwa kwa tuhuma za mauwaji.

Kontebo Edwin Oscar Okimaru ametiwa mbaroni baada ya kupatikana kuwa mshukiwa mkuu kwenye mauaji ya Joshua Mungai ambaye.

Kimaru alikamatwa jioni ya siku ya Ijumaa baada ya uchunguzi uliokuwa unafanywa na  shirika la DCI kukamilikana  kubainisha wazi kuwa mshukiwa kweli alikuwa kwenye eneo la tukio la mauaji hayo.

Jamaa yake marehemu ilikuwa imetoa ombi kwa shirika hilo kuwasaidia na uchunguzi wa kesi waliyokuwa wameandikisha katika kituo cha polisi cha Ongata Rongai.

Inadaiwa kuwa mnamo tarehe kumi na nane mwezi wa Aprili mida ya saa nne usiku, marehemu Njenga ambaye alikuwa kondakta wa matwana upande wa Ongata Rongai pamoja na marafiki wengine wawili waliotambulishwa kama Njenga na George walikamatwa kwa kukaidi sheria za amri ya kutoka nje.

Imeripotiwa kuwa watatu hau walishambuliwa na kisha kufungiwa ndani ya buti ya gari ya kibinafsi. Watatu wale walibebwa ndani ya gari hilo na kisha kutwa katika daraja la Tuala.

Hata hivyo, George aliweza kujinufungua kamba alizokuwa amefungwa na zo na kisha kuwanusuru wenzake ambao walikuwwa wamejeruhiwa vibaya.

George aliweza kuona na kusimamisha bodaboda lilikowa linapita na pamoja wakamsaidia marehemu kuabiri ingawaje mwendeshaji bodaboda yule hangeweza kumsaidia hadi hospitali kwa kuogopa kupatana na washukiwa wawili waliokuwa wamewapiga vibaya.

Marehemu aliachwa karibu na chuo kikuu cha Nazarene usiku mzima hadi msamaria mwema akamsaidia kufika kituo cha afya cha Ongata Rongai ambapo alipewa huduma ya kwanza na kisha kuhamishwa hadi hospitali kuu ya Kenyatta akiwa hali mahututi.

Siku mbili baadae marehemu aliiga dunia akipokea matibabu. Uchunguzi umebaini kuwa marehemu aliaga kutoka na majereha kifuani. Mungai pia alikuwa amevunjwa mbavu na mifupa kadhaa ishara kuwa alikuwa ameshambuliwa na kunyanyaswa.