logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gavana Waiguru akosoa kutawazwa kwa Muturi kuwa msemaji wa Gema

Gavana Waiguru akosoa kutawazwa kwa Muturi kuwa msemaji wa Gema

image
na Radio Jambo

Habari21 May 2021 - 07:07

Muhtasari


• Waiguru alisema kuwa hafla ile haitampa Muturi uongozi wa Mt Kenya kwani hiyo ni tamaduni iliyoletwa na wakoloni.

• Hafla ya kumtawaza Muturi inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi katika hekalu ya Mukurwe wa Nyagathanga.

Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga, Anne Waiguru  amekosoa vikali hatua ya kumtawaza spika wa bunge la Kitaifa Justin Muturi kuwa msemaji wa jamii za eneo la Mlima Kenya.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook na Twitter, gavana huyo alisema kuwa hafla kama ile haina maana kubwa sana kwenye siasa za eneo hilo.

"Ingawa mtu hawezi mchukia Muturi na wengine kwa tamaa utakaso bila ya mashauriano na viongozi na wakazi wa Mt Kenya, shughuli kama ile haina maana kubwa kwenye siasa" Waiguru alisema.

the star

Waiguru alisema kuwa hafla ile haitampa Muturi uongozi wa Mt Kenya kwani hiyo ni tamaduni iliyoletwa na wakoloni.

"Sharti Muturi na wengine wanaotafuta uongozi wa Mt Kenya ama kwingineko kwenda kwa wananchi na kuomba kura kwa wananchi wanaoamua nani atakuwa kiongozi wao" Waiguru alisema.

Kwa kuongeza alisema kuwa rais Kenyatta ambaye ndiye kiongozi wa Mt Kenya bado hajakiacha kiti chake na kitamaduni watu huwa hawarithi kiti wakati kiongozi bado yu hai.

Hafla ya kumtawaza Muturi inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi katika hekalu ya Mukurwe wa Nyagathanga.

Mhariri: Davis Ojiambo


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved