Mbunge wa Malindi, Bi Aisha Jumwa amekanusha madai kuwa bintiye alijiua kwa kujitia kitanzi akiwa shuleni.
Jumwa amewataka Wakenya kutupilia mbali madai hayo huku akiwaagiza wanamitandao kuepuka kueneza propaganda kutokana na uvumi usio na msingi.
Jumwa alikuwa akizungumza akiwa katika eneo bunge lake siku ya Jumamosi.
Ignore any malicious rumors doing rounds on social media, that a member of my family has committed suicide. I want to categorically state that all members of my family are safe and sound.
— Hon. Aisha Jumwa, Malindi MP. (@HonJumwa) May 22, 2021
Let’s shun propagandist agenda and baseless rumor-mongering. pic.twitter.com/1rCpAkPa5q
“Sisi wote ni wazima, msichana wangu ni mzima na tunamshukuru Mungu kwa ajili ya afya yake. Hizi zinazotembea katika mitandao ni propaganda tu” Jumwa alisema.
Ilidaiwa kuwa mwanawe Jumwa, Melisa Katana alijitia kitanzi akiwa katika shule ya upili ya Kalimoni na mwili wake kupatikana kwenye ukumbi wa kulia. Picha ya msichana aliyemfanana sana mbunge huyo iliwekwa chini ya ripoti hizo zilizosambazwa mtandaoni jambo ambalo ripoti hiyo kuaminika.
Hata hivyo, ripoti zinaarifu kuwa tukio hilo lilifanyika nchini Ghana ila si bintiye Jumwa kama ilivyodaiwa.