SIASA ZA GEMA

Wa Iria akashifu kutawazwa kwa Justin Muturi

Gavana wa Murang'a alisema kanuni za hekalu ya Mukurwe wa Nyagathanga zilikiukwa na sharti ibada ya kuitakasa ifanyike

Muhtasari

•Gavana wa Murang'a alisema kanuni za hekalu ya Mukurwe wa Nyagathanga zilikiukwa na sharti ibada ya kuitakasa ifanyike

•Mwangi alisema kuwa jamii ya GEMA inalazimishwa kumpokea kiongozi ambaye hawajamteua

Murang.a.governor.Mwangi.wa.Iria.addresing.journalists.on.Wednesday
Murang.a.governor.Mwangi.wa.Iria.addresing.journalists.on.Wednesday
Image: FILE

Spika wa bunge la kitaifa, Justin Muturi ametangaza kuwa yuko tayari kufikia viongozi wengine wa eneo la Mt Kenya na kujadiliana namna ya kuhakikisha kuwa maslahi ya eneo hilo yametimizwa.

Muturi amewapongeza wazee na viongozi walioshirikiana kuhakikisha kuwa ametawazwa kuwa msemaji wa GEMA na kusema kuwa ako tayari kuongoza.

“Nimenyenyekea sana kwa jukumu nililopewa la kuwa msemaji wa eneo la Mt Kenya. Nawashukuru wazeee wote na viongozi ambao wameshirikiana kuona kwamba jambo hili limefanikiwa na kwa kuniaminia kueleza ajenda za eneo hili” Muturi aliandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Hafla ya kumtawaza Muturi ilifanyika katika hekalu ya Mukurwe wa Nyagathanga.

Hata hivyo, uteuzi wake kuwa sauti ya eneo hilo umeendelea kusutwa sana na baadhi ya viongozi kutoka eneo hilo ikwemo gavana Mwangi wa Iria wa kaunti ya Muranga.

“Nasikitika sana kwa niaba ya jamii yangu ya Wakikuyu kwa sababu hafla iliyokuwa na ugomvi mwingi na wazee kukosana ilifanyika huku imesimamiwa na polisi. Sisi tumekataa, Mungu wa Gikuyu hawezi tishiwa na bunduki. Tunataka mahala pale patakaswe na nimeomba wazee waniruhusu tuongozee hafla ya kutakasa hekalu ya Mukurwe ili tusije tukapata shida” Mwangi alisema.

Mwangi alisema kuwa jamii ya GEMA inalazimishwa kumpokea kiongozi ambaye hawajamteua. Alisisitiza kuwa kiongozi wanaomtambua ni rais Uhuru Kenyatta.