MAUAJI BUDALANGI

Budalangi: Baba aua mwanawe wa miaka 3 na kisha kujisalimisha

Bwirre Mallo, 29, kutoka kijiji cha Sisenye alimpiga mwanawe wa miaka 3 hadi kufa kwa kula samaki bila ruhusa

Muhtasari

•Bwirre Mallo alimpiga mwanawe kwa jina Fredrick Mallo kwa sababu ya kuchukua samaki na kula bila ruhusa

• Babake mshukiwa amedai kuwa kifo cha mtoto yule kingezuiliwa iwapo angepata usaidizi mapema baada yake kupiga ripoti mara kadhaa.

crime scene 1
crime scene 1

Mwanaume mmoja wa miaka 29  katika eneo la Budalangi alijisalimisha kwa kituo cha polisi cha Port Victoria  baada ya kumpiga mtoto wake wa miaka 3 hadi akakata roho usiku wa Jumapili.

Inadaiwa kuwa Victor Bwire Mallo, 29, alimpiga mwanawe kwa jina Fredrick Mallo kwa sababu ya kuchukua samaki na kula bila ruhusa.

Mama wa kambo wa mtoto yule, Phaustine Atieno, amesimulia kuwa alikuwa ameenda kufua mtoni  tukio hilo lilipotokea.

“Nilipotoka mtoni nilipata mtoto amelala nikamuuliza shida ni nini ndipo akanieleza kuwa alikuwa amechapwa na babake kwa kula chakula, nikauliza babake akanieleza kuwa alikuwa amempiga kidogo” Atieno alisimulia.

Atieno alieleza kuwa baadaye alipika chakula na kumpa mtoto kisha akalala.

Mwendo wa saa moja nilienda kumwangalia mtoto nikaskia mguu ni baridi na nzito” Atieno alieleza.

Babake mshukiwa, Fredrick Malo ameeleza ni mazoea ya Bwire kumpiga mtoto yule na bibi yake vibaya. Amesema kuwa alijaribu kuripoti mwanawe huyo kwa msaidizi wa chifu na maafisa watawala katika eneo hilo  ila hakusaidika. Amedai kuwa kifocha mtoto yule kingezuiliwa iwapo angepata usidizi mapema baada ya kupiga  ripoti mara kadhaa.