Kiambaa: Mgombeaji aliyejiondoa Jubilee arejea baada ya kulala UDA usiku mmoja

Damaris Wambui alikuwa ametangaza kujiondoa kwenye chama cha Jubilee baada ya kutoteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mdogo ujao

Muhtasari

″Nimefukuzwa kama mbwa na nina machungu mengi sana kwa sababu nimehudumia chama cha Jubilee tangu enzi za TNA na sijawahi gombea kiti tena lakini ikifikia ni wakati wetu vijana kugombea tunaambiwa kuwa hatuna uwezo. Ni kusema kuwa katika chama cha Jubilee kijana hana nafasi” Damaris alikuwa amesema.

Damaris Wambui Waiganjo
Damaris Wambui Waiganjo
Image: Hisani

Mgombeaji wa Ki Damaris Wambui Waiganjo alirejea kwenye chama cha Jubilee baada ya usiku moja tu

Usiku wa Jumamosi baada ya kutangazwa kwa mshindi wa mahojiano ya kuamua nani atapeperusha bendera ya Jubilee Kiambaa, Damaris alikuwa ameeleza masikitiko yake kutokana na kutoteuliwa. Damaris aliibuka wa pili huku Kariri Njama akishinda uteuzi huo.

“Nimefukuzwa kama mbwa na nina machungu mengi sana kwa sababu nimehudumia chama cha Jubilee tangu enzi za TNA na sijawahi gombea kiti tena lakini ikifikia ni wakati wetu vijana kugombea tunaambiwa kuwa hatuna uwezo. Ni kusema kuwa katika chama cha Jubilee kijana hana nafasi” Damaris alieleza huku akitangaza kujiondoa kwake.

Damaris alikuwa amesuta chama cha Jubilee kwa kutopatia vijana na wanawake nafasi huku akiita cha hicho ‘chama cha wazee.’ Alikuwa ametangaza kuunga mkono mgombea kiti na chama cha UDA, John Njuguna Wanjiku.

Damaris Wanjiku akitangaza kujiondoa Jubilee
Damaris Wanjiku akitangaza kujiondoa Jubilee
Image: Hisani
Damaris Wanjiku akitangaza kujiondoa Jubilee
Damaris Wanjiku akitangaza kujiondoa Jubilee
Image: Hisani

Hata hivyo, siku ya Jumapili Damaris alifanya mkutano na wanahabari na kutangaza kubadili mawazo kwani alifanya maamuzi ya haraka na ya hasira. Alieleza kuwa alikuwa amejirudia na kuskiza ushauri kutoka kwa familia, waunga mkono, viongozi na washauri waliomsihi kubadili msimamo tena.

“Baada ya kutafuta nafsi na kupata mawaidha kutoka kwa wanaoniunga mkono, familia na washauri wangu wa kisiasa, nimeamua kuondoa maneno niliyoyasema jana kuwa nimejiondoa Jubilee. Nitabaki kwa chama cha Jubilee na kuendelea kuunga mawazo ya rais mkono na nitahakikisha kuwa chama hiki kitafaulu kwenye chaguzi ndogo zijazo Kiambaa na wadi ya Muguga” Damaris alisema.

Damaris alikuwa ameandamwa na aliyekuwa mbunge wa Dagoretti na ambaye ni mwenye kiti wa kamati ya BBI, Dennis Waweru na gavana wa kaunti ya Kiambu, James Nyoro kati ya viongozi wengine