SIASA ZA JUBILEE

Chama cha Jubilee chamteua Njama kupeperusha bendera Kiambaa

Kariri Njama atapambana na Raymond Kuria wa PEP, John Njuguna wa UDA kati ya wengine baaada ya kuibuka mshindi kwenye uteuzi uliofanyika kwa njia ya mahojiano

Muhtasari

•Uteuzi wa wagombeaji ulifanyika kwa njia ya mahojiano ya moja kwa moja

•Wagombeaji watano walihojiwa

Kariri Njama
Kariri Njama
Image: Hisani

Chama tawala cha Jubilee kimemteua Kariri Njama kupeperusha bendera kwenye uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Kiambaa.

Njama ameteuliwa baada ya kuibuka mshindi wa mahojiano yaliyofanyika katika ofisi za Jubilee zilizoko Pangani siku ya Jumamosi.

Mahojiano hayo yalishirikisha wagombeaji watano ikiwemo Josphat Gichuhi, Lenah Koinange, June Koinange, Damaris Wambui na Njama ambaye aliibuka wa kwanza akifuatwa na Damaris. Wafuasi wa wagombeaji hao waliwaandama na kungoja matokeo nje ya ofisi za Jubilee.

Katibu Mkuu wa chama hicho cha Jubilee alihakikishia wafuasi wa wagombeaji hao kuwa shughuli ile ilifanywa kwa haki.

Njama atamenyana na Raymond Kuria wa People Empowerment Party(PEP) na John Njuguna Wanjiku wa United Democratic Party (PEP) kati ya wengine katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 15 Julai.