SIASA ZA MURANGA

Kangata akashifu serikali ya kaunti kwa kusitisha kambi za matibabu

Serikali ya kaunti ya Muranga imemuagiza seneta Kangata kusitisha huduma za kambi za matibabu kutokana na janga la COVID 19

Muhtasari

•Serikali ya kaunti ya Muranga imemuagiza seneta Kangata kusitisha huduma za kambi za matibabu kutokana na janga la COVID 19

Kangata
Kangata

Seneta wa Murang’a, Irungu Kang’ata amekashifu kitendo cha serikali ya kaunti kujaribu kusitisha kambi zake za matibu.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Twitter, Kangata ametaja tendo hilo kuwa haramu;.

“Nia ya serikali ya kaunti ya Murang’a kusitisha kambi zangu za matibabu ni haramu. Hii ni kukiuka haki za wagonjwa wanyonge kwa kuwanyima matibabu bure ya hali ya juu yanayosaidia yale ya hospitali za kaunti” Kang’ata aliandika.

Kangata alikuwa anasema haya kutokana na barua ya kusitisha huduma hizo aliyopokea siku ya Alhamisi kutoka kwa waziri wa afya katika kaunti ya Muranga, Joseph Mbai.

Kwa upande wa serikali ya kaunti hiyo, Mbai alieleza kuwa huduma zile zilikuwa zimesitishwa kutokana na janga la COVID 19.