UTEUZI WA WANAFUNZI

Uteuzi wa wanafunzi katika kidato cha kwanza waahirishwa

Waliohitimu kujiunga na vyuo vikuu kwa usimamizi wa serikali waagizwa kupitia tena chaguo zao ili waweze kutengewa nafasi katika chuo Julai, 160,000 wamepewa nafasi katika vyuo vikuu vya umma na za kibinafsi.

Muhtasari

•Waziri Magoha hakupeana sababu ya kuahirisha shughuli ya uteuzi

•Watahiniwa 160,000 wa KCSE wamepewa nafasi katika vyuo vikuu vya umma na vya kibinafsi.

CS magoha
CS magoha

Wizara ya elimu nchini imeahirisha shughuli ya kuwateua wanafunzi wa kidato cha kwanza iliyokuwa imetarajiwa kufanyika kati ya tarehe 28 Mei hadi tarehe 15 Julai.

Ingawa hakupeana sababu yoyote ya tukio hilo, waziri wa elimu, George Magoha amesema kuwa hamna haja ya kuwa na hofu kwani shughuli ile ingetengewa wakati wake.

Akiizungumza katika shule ya msingi ya Joseph Kang’ethe, Magoha amehakikishia wazazi na wanafunzikuwa shughuli hiyo itakuwa ya haki.

Upande mwingine, shughuli ya kuwateua wanafunzi waliofanya mtihani wa KCSE katika vyuo vya ufundi imeanza leo.

Waliohitimu kujiunga na vyuo vikuu kwa usimamizi wa serikali wameagizwa kupitia tena chaguo zao ili waweze kutengewa nafasi katika chuo kikuu mwezi wa Julai. Watahiniwa 160,000 wamepewa nafasi katika vyuo vikuu vya umma na za kibinafsi.