UFISADI WA ARROR NA KIMWARER

Rotich ashtakiwa upya kwenye kashfa ya Kimwarer na Arror

Kwenye mashtaka mapya , upande wa mashtaka umeondoa majina ya katibu mkuu, Kamau Thugge na Susan Koech ambao walikubali kutoa ushahidi wao

Muhtasari

•Kwenye mashtaka mapya , upande wa mashtaka umeondoa majina ya katibu mkuu, Kamau Thugge na Susan Koech ambao walikubali kutoa ushahidi wao

Henry Rotich mahakamani
Henry Rotich mahakamani
Image: Maktaba

Aliyekuwa waziri wa hazina, Henry Rotich amekanusha mashtaka ya kuhusika kwenye wizi wa mabilioni ya pesa kutokana na mradi wa ujenzi wa mabwawa ya Arror na Kimwarer baada ya kushtakiwa upya.

Rotich alisomewa karatasi mpya ya mashtaka baada ya marekebisho kufanywa kwa karatasi ile ya kwanza na mkurugenzi wa mashtaka ya umma(DPP). Mashtaka hayo yalisomwa mbele ya hakimu mkuu,Douglas Ogoti.

Kwenye karatasi hiyo mpya, upande wa mashtaka umeondoa majina ya katibu mkee, Kamau Thugge na Susan Koech ambao walikubali kutoa ushahidi wao .

DPP pia ameondoa majina ya Waitaliano 20 ambao walikuwa wamehusishwa kwenye kesi hiyo kwani bado hawajulikani waliko. Watasomewa mashtaka yao kando.

Rotich pamoja na wengine walioshtakiwa naye wamekanusha mashtaka yote huku DPP akisema kuwa ushahidi uliotolewa kwenye kesi hiyo utabaki vile vile na hawatatoa hati zingine ama kuleta mashahidi wapya.

Kwa sasa kuna kesi mbili zinaendelea na tumekiri kuwa hatuna nia yoyote ya kuziunganisha ata kama washukiwa wengine wanaohusishwa ni walewale. Wengi kati yao ni watu tofauti kwenye kesi hizo mbili” upande wa mashtaka ulisema.

Mahakama sasa ina kesi tatu zinazohusiana na wizi wa Arror na Kimwarer.