MAUAJI NAKURU

Mwanaume aomboleza bibi, mtoto na mfanyikazi Nakuru

Mwalimu , mwanawe wa miaka 3 na mfanyikazi waligongwa kwa vifaa butu, wakanyongwa na kuachwa kuteketea huku mtoto mchanga akiponea na majeraha

Muhtasari

•Naibu kamanda wa polisi katika eneo kaunti ya Nakuru, Joseph Tonui  alisema kuwa waliotekeleza mauaji hayo walitaka kuteketeza nyumba hiyo ili kuficha ushahidi. Alisema kuwa miili ya watatu hao ilipatikana katika harakati ya majirani kuzima moto uliokuwa umewashwa kuteketeza nyumba ile.

crime scene 1
crime scene 1

Mwanaume mmoja mkazi wa eneo la Mzee wa Nyama iliyo katika viunga vya Nakuru  anaomboleza kumpoteza bibi, mtoto wa miaka 5 na mfanyikazi  kwa mauaji ya kinyama jioni  ya Jumatano.

Inadaiwa kuwa Alice Njeri ambaye ni mwalimu katika shule ya Maria Mtakatifu, mwanawe mmoja mvulana wa miaka 5 na mfanyikazi wao Ann Wangari wa miaka 44 walipatika ndani ya nyumba yao iliyokuwa inatekeketea wakiwa wameaga.

Alitutayarishia chai vizuri akaacha tukikunywa na watoto asubuhi. Mimi nimeshinda kazini mchana mzima sijampigia simu. Mwendo wa kumi na mbili hivi nikitokea kazini nimepigiwa simu nikaelezwa nikimbie hapa nyumbani. Wakati nimefika nikaambiwa kwamba nyumba imechomeka.. nikapata mke wangu ameuawa, mwajiriwa wake na pamoja na mtoto wote wameuawa” Mume huyo alisimulia.

Mtoto mmoja aliyekuwa amejeruhiwa alipatikana akilia kwenye kiti . Majirani waliweza kumuokoa.

Akithibitisha tukio hilo, naibu kamanda wa polisi katika eneo kaunti ya Nakuru, Joseph Tonui  alisema kuwa waliotekeleza mauaji hayo walitaka kuteketeza nyumba hiyo ili kuficha ushahidi. Alisema kuwa miili ya watatu hao ilipatikana katika harakati ya majirani kuzima moto uliokuwa umewashwa kuteketeza nyumba ile.

Imeripotiwa kuwa watatu hao waligongwa na vifaa butu , wakanyongwa, wakadungwa kwa visu kisha kuachwa kuteketea kwa nyumba. Mwili wa mfanyikazi ulipatikana jikoni alikokuwa akipika huku miili ya Njeri na mwanawe ikipatikana sebuleni.

Tulipata moto ikiwaka tukaanza kumwaga maji. Katika harakati ya kumwaga maji tukapata mtoto  mmoja aliyekuwa amenyongwa akawachwa hapo kwa kiti na mwingine mchanga kidogo, wa kama mwaka moja na nusu hivi alikuwa hai na hakuwa amefungwa japo hangeweza kujiokoa” mmoja wa walioshuhudia tukio hilo alieleza.

Inadaiwa kuwa familia hiyoilikuwa imehamia nyumba hiyo siku kumi na mbili tu kabla ya mkasa huo kutokea