WIZI BARABARANI

Majambazi 6 wakamatwa kwa kuvamia waendesha magari kwenye barabara ya Southern Bypass

Inadaiwa kuwa Tom Onyango alliegesha gari ili kumruhusu mwanawe kuenda haja ndipo wakavamiwa na majambazi hao ambao walikuwa wamejihami vilivyo

Muhtasari

•Tom Onyango alikuwa ameegesha garil ili kumruhusu mwanawe kuenda haja

•Onyango aliweza kutambua watatu kati ya sita waliokamatwa kuwa walihusika katika wizi huo

crime scene
crime scene

Majambazi sita ambao wamekuwa wakiwavamia na kuwaibia bidhaa za thamani waendesha magari katika barabara ya Southern Bypass wamekamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Lang'ata.

Sita hao walikamatwa baada ya kumuibia mwanaume mmoja aliyekuwa anasafiri na mwanawe kutoka Nakuru hadi Nairobi.

Inadaiwa kuwa Tom Onyango alisimamisha gari ili kumruhusu mwanawe kuenda haja walipovamiwa na majambazi hao ambao walikuwa wamejihami kabisa.

Punde baada ya wizi huo kufanyika, Onyango alipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Lang'ata. Maafisa wa usalama wakisaidiwa na mbwa wa kufuatiliawa walianza shuguli ya kuwatafuta majambazi wale waliokuwa wamejificha msituni.

Maafisa wale waliweza kuwachomoa washukiwa sita kutoka msituni huo, watatu wao ambao waliweza kutambulikawa na Onyango kuwa waliowavamia.

Idara ya DCI imewaagiza waendeshaji magari ambao wamevamiwa kwenye barabara hiyo hapo awali kupiga ripoti katika kituo cha polisi cha Lang'ata ili kuwasaidia katika uchunguzi.